Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Joseph Anania Tadayo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwanga
Primary Question
MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza:- Je, Serikali kupitia TARURA ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Mangio hadi Kivizini Wilayani Mwanga?
Supplementary Question 1
MHE. JOSEPH A. TADAYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali kwenye swali hili la msingi, lakini nina swali moja la nyongeza lenye (a) na (b).
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuuliza tu kwamba ni lini Serikali itakarabati kwa ukamilifu Barabara za (a) Masumbeni - Butu na (b) Msangeni – Butu ikizingatiwa kwamba barabara hizi zinaelekea maeneo yanayotegemewa kwa uzalishaji wa chakula na Serikali imewekeza mabilioni ya fedha kwenye miradi ya umwagiliaji, lakini barabara hazipitiki mwaka mzima? Ahsante. (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niendelee kumpa taarifa Mheshimiwa Mbunge kwamba, Serikali ya Awamu ya Sita inatambua umuhimu mkubwa sana wa barabara zetu hizi za Wilaya zinazosimamiwa na TARURA. Umuhimu wake ni mkubwa kiuchumi kwa maana ya kuwawezesha wananchi kufanya shughuli zao mbalimbali za uchumi ikiwemo kilimo na kuwawezesha wananchi kuweza kufikia huduma za msingi za kijamii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha miaka minne cha Serikali ya Awamu ya Sita, Shilingi bilioni 12.05 zimetumika kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya barabara katika Wilaya hii ya Mwanga. Pia, katika mwaka huu wa bajeti wa 2024/2025, shilingi bilioni 5.2 zimetengwa kwa ajili ya kuhakikisha zinaendelea kuimarisha barabara hizi muhimu kabisa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niendelee kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge, barabara hizi mbili alizozitaja Serikali itazifikia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba zinajengwa na zinapitika katika kipindi cha mwaka mzima ili kuweza kuwanufaisha wananchi kiuchumi kwa maana ya shughuli zao za kilimo na shughuli mbalimbali za uchumi wanazozifanya, lakini pia kuwawezesha kufikia huduma za msingi za kijamii. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge umewasemea wananchi wako na Serikali ya Awamu ya Sita imekusikia na itafika kuja kuleta maendeleo hayo kwa ajili ya wananchi wako. (Makofi)
Name
Shabani Omari Shekilindi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lushoto
Primary Question
MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza:- Je, Serikali kupitia TARURA ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Mangio hadi Kivizini Wilayani Mwanga?
Supplementary Question 2
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika Jimbo la Lushoto zimeharibu miundombinu ya barabara hasa Barabara ya Malibwi - Kwekanga hadi Makole. Mpaka ninavyoongea sasa hivi wananchi wana miezi miwili hawapati huduma. Je, nini mpango wa Serikali wa dharura kutengeneza barabara zile ili wananchi wangu waendelee kupata huduma hiyo? Ninakushukuru.
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikichukua hatua za dharura kuweza kurudisha mawasiliano kwenye barabara ambazo mawasiliano yamekatika. Serikali imekuwa ikiendelea pia kuimarisha barabara zetu za Wilaya kuhakikisha kwamba zinakuwa katika mazingira ambayo zinaweza kupitika katika kipindi cha mwaka mzima ili kuweza kuwanufaisha wananchi, kwa maana ya kuwawezesha kufanya shughuli zao za uchumi na kufikia huduma za msingi za kijamii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Mwaka huu wa Fedha 2024/2025 kuna bilioni 21 ambazo zimetengwa kwa ajili ya dharura, kuhudumia barabara zetu hizi za TARURA kwa dharura. Pia Bunge hili Tukufu lilipitisha nyongeza ya bajeti bilioni 50 kwa ajili ya kuhudumia barabara hizi ambazo zinaharibika kwa utaratibu wa dharura. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, tutafika katika eneo alilolitaja.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatumia nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, kumwagiza Meneja wa TARURA wa Mkoa akishirikiana na Meneja wa TARURA wa Wilaya waweze kufika katika eneo alilolitaja Mheshimiwa Mbunge, kufanya tathmini na kuleta kwenye mipango ili eneo hilo liweze kupatiwa huduma ya kurudisha mawasiliano ili barabara hii iweze kuwanufaisha wananchi. (Makofi)
Name
Nancy Hassan Nyalusi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza:- Je, Serikali kupitia TARURA ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Mangio hadi Kivizini Wilayani Mwanga?
Supplementary Question 3
MHE. NANCY H. NYALUSI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Barabara ya Mdabulo - Ihanu ni barabara inayotegemewa na wananchi katika shughuli zao za kiuchumi. Je, ni lini Serikali itafanya maboresho katika barabara hiyo?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Awamu ya Sita imeweka kipaumbele kikubwa sana katika kuimarisha barabara zetu hizi za Wilaya zinazosimamiwa na TARURA, ndiyo maana utaona tangu Awamu ya Sita imeanza kufanya kazi utaona bajeti ya TARURA imeongezeka mara dufu kutoka bilioni 275 kila mwaka, mpaka sasa tunatarajia bajeti ya TARURA katika mwaka wa fedha ujao 2025/2026 itakuwa ni shilingi trilioni 1.18.
Mheshimiwa Mwenyekiti, dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita unaiona kwa nyongeza hii ya bajeti. Ninaomba niendelee kumhakikishia Mheshimiwa kwamba, Serikali itafika kwenye barabara aliyoitaja kwa ajili ya kuhakikisha kwamba inaendelea kuiboresha, kuiweka katika hadhi ambayo itapitika mwaka mzima ili iweze kuwanufaisha wananchi kiuchumi na iwawezeshe waweze kufikia huduma za msingi kabisa za kijamii. Kwa hiyo, ninaomba Mheshimiwa Nancy upokee taarifa hiyo, Serikali itafika. (Makofi)
Name
Hussein Nassor Amar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nyang'hwale
Primary Question
MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza:- Je, Serikali kupitia TARURA ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Mangio hadi Kivizini Wilayani Mwanga?
Supplementary Question 4
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, barabara za mitaa kwenye Makao Makuu ya Wilaya pale Karumwa zimeharibika. Je, upo tayari kumwelekeza Meneja wa TARURA Nyang’hwale aweze kuzifungua barabara hizo za Mtaa wa Mahango, Marekana, Bubapa, Busengwa pamoja Butaranda? Ahsante. (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kuendelea kuimarisha barabara zetu hizi za wilaya ambazo zinasimamiwa na TARURA, ndiyo maana utaiona dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhakikisha hivyo na ndiyo maana kila mwaka bajeti inaendelea kuongezeka.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nitumie fursa hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), kumwagiza Meneja wa TARURA wa Mkoa akishirikiana na Meneja wa TARURA wa Wilaya kuweza kuzifanyia tathmini barabara hizi katika mitaa ambayo ameitaja Mheshimiwa Hussein Amar ili ziweze kuwepo katika mpango kwa ajili ya kuja kuhakikisha kwamba zinapatiwa fedha na zinakarabatiwa ziwe katika hadhi nzuri na ziweze kuwanufaisha wananchi wa Jimbo lake.
Name
Josephine Johnson Genzabuke
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza:- Je, Serikali kupitia TARURA ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Mangio hadi Kivizini Wilayani Mwanga?
Supplementary Question 5
MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Halmashauri ya Kibondo, barabara ya kutoka Kibondo Mjini kwenda Kumhasha imeharibika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika Halmashauri ya Kibondo. Je, Serikali ipo tayari kutengeneza barabara hiyo ambayo ni muhimu sana kwa wananchi wanaotoa bidhaa kutoka shambani kuleta Mjini Kibondo? Ahsante. (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikifanya jitihada za dharura na mpango wa muda mrefu Serikali inaendelea kukarabati na kuhakikisha barabara hizi zinakuwa katika hadhi nzuri kuwawezesha wananchi kufanya shughuli zao za kiuchumi na kufikia huduma za msingi za kijamii.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niendelee kumhakikishia Mheshimiwa Josephine Genzabuke kwamba, dhamira ya Serikali ya kuendelea kuimarisha barabara zetu za Wilaya ipo pale pale na ipo kwa vitendo na barabara hizi ulizozitaja na hasa hii katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo zitafikiwa kwa ajili ya kuhakikisha kwamba zinaimarishwa na zinaweza kupitika katika kipindi cha mwaka mzima na hatua za dharura kuchukuliwa kwenye maeneo ambayo mawasiliano yamekatika ili wananchi waweze kuendelea na shughuli zao za kiuchumi na waweze kufikia huduma za kimsingi za kijamii. (Makofi)