Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 17 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 212 2025-05-05

Name

Joseph Anania Tadayo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanga

Primary Question

MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza:-

Je, Serikali kupitia TARURA ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Mangio hadi Kivizini Wilayani Mwanga?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Mangio hadi Kivisini yenye urefu wa kilometa 7.1 inapatikana ukanda wa milimani katika Wilaya ya Mwanga. Kwa sasa TARURA inaendelea na usanifu wa barabara hiyo ambapo utakapokamilika na makisio ya gharama kufahamika itawekwa kwenye mipango ya bajeti kwa ajili ya utekelezaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kuhudumia mtandao wa barabara na madaraja katika Wilaya ya Mwanga kwa kujenga, kukarabati na kufanya matengenezo kulingana na upatikanaji wa fedha.