Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Amb. Liberata Rutageruka Mulamula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nominated
Primary Question
MHE. BALOZI LIBERATA R. MULAMULA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kukarabati Shule Kongwe za Msingi na Sekondari – Missenyi?
Supplementary Question 1
MHE. BALOZI LIBERATA R. MULAMULA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina swali la nyongeza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Missenyi imekuwa ikiahidi kufanya tathmini ya hali ya majengo haya yaliyochakaa sana hususan Shule ya Msingi ya Novati Rutageruka ambayo bahati nzuri au mbaya imeitwa jina la marehemu mzee wangu iliyopo Kijiji cha Kitobo ambayo kwa kweli hali yake ni mbaya sana na inahatarisha maisha ya wanafunzi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Naibu Waziri nilishampelekea clip hiyo na kwa kweli ninaomba ipewe kipaumbele hali ni mbaya mno na miundombinu imechakaa sana. Kwa hiyo, ninaomba sasa Serikali itupie jicho hilo na ikibidi Naibu Waziri twende wote Waziri akaone hiyo, maana yake ninaona kama video clip haikutosha, ninaomba twende wote akaone hali halisi. Ahsante sana. (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
MWENYEKITI: Ahsante sana Mheshimiwa Balozi, ninaamini kabisa Mheshimiwa Waziri ameyachukua hayo na atayafanyia kazi kwa namna ambavyo ameomba.
Name
Aysharose Ndogholi Mattembe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. BALOZI LIBERATA R. MULAMULA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kukarabati Shule Kongwe za Msingi na Sekondari – Missenyi?
Supplementary Question 2
MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa nafasi. Je, ni lini Serikali itakarabati Shule ya Sekondari Mrama katika Jimbo la Singida Kaskazini hasa ukizingatia ni chakavu na ni kongwe sana? (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua kuna shule ambazo zimejengwa hata kabla ya nchi yetu kupata uhuru na shule hizi hasa shule za msingi ni shule kongwe na ni chakavu. Serikali imekuwa ikitenga fedha kila mwaka kwa ajili ya kuhakikisha inazifikia shule hizi kwa awamu kwa ajili ya kuzikarabati ili ziwe katika hali nzuri na ziweze kutoa mazingira mazuri zaidi ya wanafunzi wetu kusoma na mazingira mazuri zaidi kwa ajili ya walimu kufundishia.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Aysharose Mattembe, kwamba katika jitihada zile za Serikali kuendelea kuzifikia shule hizi kongwe, shule aliyoitaja itafikiwa kwa ajili ya kukarabatiwa ili iwe katika hadhi nzuri iendane na shule nyingine ambazo Serikali inaendelea kuzijenga kwa maana ya shule mpya. (Makofi)
Name
Nicodemas Henry Maganga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbogwe
Primary Question
MHE. BALOZI LIBERATA R. MULAMULA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kukarabati Shule Kongwe za Msingi na Sekondari – Missenyi?
Supplementary Question 3
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Mbogwe inazo shule nyingi ambazo zimechakaa na ni za muda mrefu tukianzia Kata ya Nanda, Kata ya Ilolwangulu pamoja na Ushirika. Serikali ina mpango gani kutoa pesa ili shule zile ziweze kukarabatiwa? Ahsante. (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, kila mwaka wa fedha, Serikali hasa hii ya Awamu ya Sita imekuwa ikitoa fedha nyingi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba inaboresha miundombinu katika Sekta ya Elimu. Katika kipindi cha miaka minne tu ya Serikali ya Awamu ya Sita tayari shilingi trilioni 5.1 zimetumika katika kuimarisha Sekta hii muhimu ya Elimu Msingi kwa maana ya shule zetu, madarasa ya awali shule za msingi na shule za sekondari.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niendelee kumhakikishia Mheshimiwa Nicodemas Maganga kwamba hata katika Halmashauri ya Mbogwe, Serikali imekuwa ikifika kila mwaka wa bajeti kwa ajili ya kukarabati shule hizi kongwe. Nimhakikishie Serikali itaendelea kufanya hivyo katika kila mwaka wa bajeti tutaendelea kutenga fedha na kufikia shule hizi kongwe kwa awamu kuhakikisha kwamba na zenyewe zinakuwa katika hadhi nzuri sambamba na shule mpya ambazo kila mwaka Serikali ya Awamu ya Sita inazijenga. (Makofi)
Name
Florent Laurent Kyombo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nkenge
Primary Question
MHE. BALOZI LIBERATA R. MULAMULA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kukarabati Shule Kongwe za Msingi na Sekondari – Missenyi?
Supplementary Question 4
MHE. FLORENT L. KYOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikushukuru kwa nafasi. Kwanza, niipongeze Serikali; ndani ya Wilaya Missenyi Serikali imefanya kazi kubwa na nzuri. Tumejengewa shule mpya tatu za sekondari, shule mpya ya msingi lakini na vyumba vya madarasa zaidi ya 200. Pamoja na hayo kama alivyosema kwenye majibu ya swali la msingi bado kuna shule chakavu ambazo nazo ukarabati kama alivyosema Mheshimiwa Naibu Waziri umeendelea kwa awamu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa swali langu la msingi; je, ni lini Serikali angalau itapunguza hizo shule nyingi za msingi ambazo zimechakaa ili angalau watoto wetu waweze kusomea katika mazingira mazuri kama wenzao?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Awamu ya Sita ina dhamira ya dhati ya kuendelea kuimarisha Sekta ya Elimu na hasa elimu msingi na ndiyo maana utaona kwamba katika kipindi cha miaka minne cha Serikali ya Awamu ya Sita, shilingi trilioni 5.1 zimetumika kuimarisha miundombinu na sekta nzima ya elimu kwa ujumla wake kwa upande wa elimu msingi. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niendelee kumhakikishia Mheshimiwa Kyombo, kwamba Serikali itaendelea kuleta fedha kwa ajili ya kukarabati shule kongwe. Tunafahamu shule hizi zilijengwa hata kabla ya Tanzania hii kupata uhuru (kabla ya nchi yetu kupata uhuru). Kwa hiyo, Serikali itaendelea kuleta fedha ili kuzikarabati hizi shule.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyotangulia kusema katika mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali imetenga shilingi milioni 60 kwa ajili ya kuendelea kukarabati shule hizi ambazo ni chakavu. Pia, Mheshimiwa Mbunge umekuwa ukipaza sauti yako sana kutaka kuhakikisha kwamba miundombinu hii katika Sekta ya Elimu inaimarishwa katika Jimbo lako ukiwasemea wananchi wako. (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2024/2025, imetengwa shilingi milioni 157.7 kwa ajili ya kwenda kukarabati Shule ya Msingi Noveti. Pia, shule ile itajengewa madarasa matano, kutakuwa na vyumba viwili vya madarasa ya awali vile vya mfano na kutakuwa kuna matundu ya vyoo 12. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge ninaomba ukae mkao wa kupokea neema hiyo kubwa inayoletwa na Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Jimbo lako la Missenyi. (Makofi)