Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 17 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 211 2025-05-05

Name

Amb. Liberata Rutageruka Mulamula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Primary Question

MHE. BALOZI LIBERATA R. MULAMULA aliuliza:-

Je, kuna mpango gani wa kukarabati Shule Kongwe za Msingi na Sekondari – Missenyi?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi ina shule kongwe 55 (msingi 52 na sekondari tatu). Kutokana na hali ya miundombinu ya shule hizo kuwa chakavu, Serikali imeendelea kuboresha miundombinu kwa kukarabati au kujenga miundombinu mipya kwa awamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mwaka wa Fedha 2023/2024 na 2024/2025, Serikali imetumia shilingi 182,000,000 kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya madarasa kwenye shule 11 na ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule tano katika Halmashauri ya Wilaya ya Missenyi. Aidha, Mwaka wa Fedha 2025/2026, Serikali imetenga shilingi 60,000,000 kwa ajili ya ukarabati wa vyumba chakavu vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Lugoye.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kukarabati shule chakavu za msingi na sekondari kadri ya upatikanaji wa fedha. (Makofi)