Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Stella Simon Fiyao

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza:- Je, kwa nini Wastaafu hawapewi haki zao mara tu wanapostaafu?

Supplementary Question 1

MHE. STELLA S. FIYAO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana kwa kunipa nafasi. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; kwa mujibu wa wastaafu, Serikali iliwaahidi kutoa nyongeza ya pensheni kwa kila mstaafu nchi nzima lakini jambo hili mpaka sasa halijafanyika. Ninataka kujua kauli ya Serikali ni ipi katika hili?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili; wastaafu wengi kabla ya kustaafu walijiendeleza na wakapandishwa madaraja, lakini baada ya kustaafu hawakulipwa mafao yao kutokana na yale madaraja mapya. Ninataka kujua kauli ya Serikali katika hili?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI): Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Fiyao kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nimtaarifu Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari zingatio la nyongeza ya pensheni ya wastaafu limekwisha kufanyika tangu mwezi Januari na Februari. Utekelezaji ulikwisha kuanza kutoka kima cha kiwango cha shilingi 100,000 hadi shilingi 150,000 na hii inafanyika katika pande zote kwa wale wastaafu wa Sekta Binafsi (NSSF) na wale walio katika ustaafu wa Sekta ya Umma (PSSSF).

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatambua kwamba tayari Serikali kwa maagizo mahususi ya Mheshimiwa Rais, imeendelea kuhakikisha kwamba inaboresha maslahi ya wastaafu kwenye hayo maeneo ikiwa ni pamoja na wale ambao fedha zao zinapitia Hazina. Kazi kubwa inafanyika ili kuweza kuhakikisha kwamba haki na stahiki zao wanazipata.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, amesema wastaafu wengi wanapata changamoto kuhusiana na pale wanapostaafu, lakini walikuwa wamepandishwa madaraja, ni namna gani malipo yao. Kwa sisi Ofisini mpaka sasa wastaafu wote changamoto zao zimeshughulikiwa. Kama Mheshimiwa atakuwa na orodha mahususi kwa sababu amesema wastaafu wengi, ni vizuri akalileta haraka sana kabla hata ya kuuliza swali tuweze kulishughulikia kwa sababu wanaostaafu ni watu ambao wamelitumikia Taifa hili kwa moyo lakini pia wamekuwa wazalendo na wametumikia kwa utumishi uliotukuka. Mheshimiwa Rais amesema wakati wote tuweze kuzingatia kwenye kuhakikisha kwamba tunawapa kipaumbele katika kutekeleza haki zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, hii nimwombe Mheshimiwa Mbunge kama anao atuletee hiyo orodha ili tuweze kulishughulikia mapema. Katika ofisi kwa sasa kwenye desk hakuna pending issue ya wastaafu katika suala hilo.