Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 17 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 210 2025-05-05

Name

Stella Simon Fiyao

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza:-

Je, kwa nini Wastaafu hawapewi haki zao mara tu wanapostaafu?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Stella Simon Fiyao, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la ucheleweshaji wa malipo ya mafao ya wastaafu katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa sasa limekuwa historia. Mifuko imeboresha mifumo yao ya TEHAMA, hatua ambayo imeiwezesha kulipa mafao ya wastaafu ndani ya kipindi kilichowekwa kisheria, au hata kwa muda mfupi zaidi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kusimamia kwa karibu utendaji wa Mifuko ili kuhakikisha kuwa inaendelea kuondoa vikwazo na kuwalipa wastaafu mafao yao mapema kadri inavyotakiwa. Ahsante.