Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Leah Jeremiah Komanya
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Meatu
Primary Question
MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Bwawa katika Kijiji cha Lukale na Mwabagimu Wilayani Meatu ili kuondakana na adha ya maji ya chumvi?
Supplementary Question 1
MHE. LEAH J. KOMANYA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali. Kazi kubwa imefanyika kutoka upatikanaji wa maji 40% mpaka sasa 85%. Ninaomba sasa, kwa kuwa, kuna miradi ya shilingi bilioni nne inayotekelezeka ndani ya Jimbo la Meatu, changamoto iliyopo ni upatikanaji wa fedha. Serikali iko tayari kuleta fedha ili tuweze kukamilisha miradi hiyo?
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka huu wa Bajeti 2024/2025 na mpango, Serikali imetenga shilingi bilioni 1.1 katika mradi huu alioutaja Mheshimiwa Waziri, na tumebakiza mwezi mmoja. Je, Serikali ni lini itaanza kutekeleza mradi huu?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nampongeza sana Mheshimiwa Mbunge kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya, lakini kubwa katika eneo lake, tuna miradi sita yenye thamani ya shilingi bilioni nne, ambayo iko katika hatua mbalimbali. Ninataka nimhakikishie, Wizara ya Maji imeongezewa fedha katika bajeti yake na tunatambua utekelezaji wa miradi ya maji unategemea fedha. Tutapaleka fedha kuhakikisha miradi hii inakamilika na wananchi wake wanapata huduma ya majisafi na salama.
Mheshimiwa Naibu Spika, juu ya swali la pili, sasa hivi tupo katika hatua ya upembuzi yakinifu. Ninataka niwahakikishie, ninapokamilisha, na hii miradi tutaianza, ili kuhakikisha kwamba inakamilika na wananchi hawa waweze kupata huduma hii muhimu sana ya maji. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved