Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 35 Water and Irrigation Wizara ya Maji 454 2025-05-29

Name

Leah Jeremiah Komanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Meatu

Primary Question

MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga Bwawa katika Kijiji cha Lukale na Mwabagimu Wilayani Meatu ili kuondakana na adha ya maji ya chumvi?

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ruhusa yako, ninaomba nitumie nafasi hii kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, viongozi wote wa Serikali, chama, Bunge lako Tukufu, ukiwepo wewe pamoja na Mheshimiwa Spika na Waheshimiwa Wabunge, Wananchi wa Jimbo la Pangani na Watumishi wote wa Wizara ya Maji. Tumepitia kipindi kigumu cha kuondokewa na mdogo wangu kipenzi, Ally Hamidu Aweso, nikiwa katika shughuli zangu za Bunge. Mungu anasema, “Yapaswa kushukuru kwa kila jambo.” Ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa mtihani huu mzito, lakini Mungu ailaze mahali pema Peponi roho ya Marehemu. Amina.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mpango wa muda mfupi, Serikali imekamilisha ujenzi wa bwawa dogo katika Kijiji cha Lukale, Wilayani Meatu, ambapo kupitia bwawa hilo, wananchi wanapata huduma ya maji kwa kutumia pampu ya mkono. Aidha, katika hatua nyingine, Serikali imeanza hatua za awali za ujenzi wa mabwawa ya maji katika Vijiji vya Lukale na Mwabagimu, ambapo kazi zinazofanyika kwa sasa ni utafiti wa udongo na upembuzi yakinifu ili utekelezaji wake uweze kuanza.