Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Bakar Hamad Bakar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
House of Representatives
Primary Question
MHE. BAKAR HAMAD BAKAR aliuliza: - Je, lini ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Chakechake itatekelezwa?
Supplementary Question 1
MHE. BAKAR HAMAD BAKAR: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana. Ahadi ya ujenzi wa Kituo hiki cha Wilaya ya Chakechake ni ahadi ya muda mrefu sasa. Ninataka nifahamu ni upi mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba, fedha hizi, shilingi milioni 800, zinapatikana kwa ajili ya kwenda kujenga kituo hiki? Pia, nyumba za Askari na Maafisa mbalimbali wa pale Madungu, Chakechake, ni chakavu na ni za muda mrefu sana.
NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tuko kwenye kipindi cha bajeti. Ninaomba sana muwe watulivu ndani ya Bunge. Swali Waziri halisikii, meza haikusikii, na hata Hansard watashindwa kuandika haya mahojiano ambayo yako ndani.
Mheshimiwa Waziri.
MHE. BAKAR HAMAD BAKAR: Mheshimiwa Naibu Spika, nilikuwa ninakwenda kwenye swali la pili.
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli, ahadi hiyo aliyoisema Mheshimiwa Mbunge ni ya muda mrefu, lakini kwanza tuliongeza kituo hicho kwenye mpango, na sasa, kama nilivyojibu kwenye jibu la msingi, tunatenga fedha kwenye mwaka wa fedha 2026/2027 tayari, kwa ajili ya kuanza ujenzi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali la pili la uchakavu wa nyumba za Askari, ni kweli nyumba hizo ni chakavu. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwanza tutatuma wataalamu wetu wakafanye tathmini kuhakikisha kwamba, je, tunafanya ukarabati au kujenga upya nyumba hizo? Kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, Serikali italifanyia kazi suala hilo. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved