Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 35 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 453 2025-05-29

Name

Bakar Hamad Bakar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. BAKAR HAMAD BAKAR aliuliza: -

Je, lini ahadi ya ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Chakechake itatekelezwa?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Chakechake imetoa kiwanja Na. 61 chenye ukubwa wa mita za mraba 1,429, eneo la vitongoji, kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi, Daraja “B”, cha Wilaya ya Chakechake. Ujenzi wa kituo hicho utagharimu kiasi cha shilingi 802,926,788. Fedha hizo zitatengwa kwenye Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/2027, ahsante.