Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Joseph Michael Mkundi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ukerewe
Primary Question
MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Tawi la Chuo cha Uuguzi na Uganga - Ukerewe?
Supplementary Question 1
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Naibu Spika, nianze kwa kuishukuru sana Serikali kwa kuridhia na kutoa pesa, kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Hospitali ya Rufaa kwa ngazi ya mkoa, Jimboni Ukerewe. Nina swali moja la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa, sasa tunakamilisha majengo mapya ya halmashauri yetu ya wilaya, na yale majengo yaliyokuwa yanatumika zamani yatakuwa matupu, Serikali sasa iko tayari kuja kufanya tathmini ya majengo yale na kama itaridhika, basi ianze kuyatumia, kwa ajili ya mafunzo ya wanafunzi wa uganga na uuguzi?
Name
Dr. Godwin Oloyce Mollel
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Siha
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, kama ambavyo Wizara ya Afya, mimi, yeye, pamoja na Waziri wa Afya tumekuwa tukifanya kazi, hasa kwenye eneo la hospitali, ambayo inajengwa kwenye Wilaya yake ya Ukerewe. Pia ninamwomba sasa aje, halafu Wizara itampa wataalamu kwenda Ukerewe na kuangalia hayo majengo, ili waweze kuleta ripoti. Kama inawezekana tukaanzisha chuo kwenye eneo hilo.
Mheshimiwa Naibu Spika, cha msingi kabla ya kuanzisha chuo ni lazima pawepo na hospitali ambayo itaweza kutumika kama sehemu ya kufundishia kwa sababu, majengo ni jambo moja na hospitali ambayo inaweza ikatumika kwa ajili ya kuhakikisha tunawafundisha wataalamu masomo kwa vitendo, ni muhimu kuwepo katika eneo hilo.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved