Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 35 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 452 2025-05-29

Name

Joseph Michael Mkundi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukerewe

Primary Question

MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga Tawi la Chuo cha Uuguzi na Uganga - Ukerewe?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli. Bado kuna mahitaji ya vyuo katika maeneo mbalimbali ya nchi, ila kwa sasa Serikali inajenga hospitali yenye hadhi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa katika Wilaya ya Ukerewe.

Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na ujenzi huo, Serikali itaendelea kufanya upembuzi yakinifu kuona kama eneo hilo litahitaji kuwa na Chuo cha Uuguzi mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa.

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kuwasilisha.