Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Alfred James Kimea

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Korogwe Mjini

Primary Question

MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA aliuliza: - Je, lini TANROADS itamalizia kuweka taa za barabarani katikati ya Mji wa Korogwe, kwenye Barabara Kuu itokayo Dar es Salaam hadi Arusha?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini ninaomba Waziri afahamu kwamba, Korogwe ni kati ya miji inayokua kwa kasi sana. Kutokuwepo kwa taa za barabarani, kwa baadhi ya maeneo, kunaleta changamoto kubwa. Je, wanatuambia ni lini taa hizo zitakamilika kwenye Mji wa Korogwe mzima?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyojibu katika jibu langu la msingi kwamba suala la zoezi la kuweka taa ni endelevu, kwa sababu pia, miji imeendelea kukua. Kwa hiyo, tutaendelea na utaratibu huo. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, hata katika mwaka wa fedha unaokuja 2025/2026 tumepanga kuendelea kuweka taa katika miji, ukiwepo na Mji wa Korogwe.

Name

Husna Juma Sekiboko

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA aliuliza: - Je, lini TANROADS itamalizia kuweka taa za barabarani katikati ya Mji wa Korogwe, kwenye Barabara Kuu itokayo Dar es Salaam hadi Arusha?

Supplementary Question 2

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana. Wilaya ya Lushoto, kwa mujibu wa hali ya hewa, ina ukungu sana, hasa kipindi hiki cha mwezi wa Tano, wa Sita mpaka wa Nane. Je, Serikali ina mpango gani wa kuweka taa katika Miji ya Wilaya ya Lushoto, kama Mlola, Lukozi na Mtae, ili kupunguza ukungu unaosababisha giza zito wakati wa matumizi ya barabara?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, labda nitoe tu maelezo kwamba, kwa sasa katika barabara zote mpya tunazojenga kwenye miji, tunaweka taa, lakini kwa miji ambayo ipo na haipo kwenye miradi, kwanza katika bajeti tumehakikisha kwamba, kila mkoa utatengewa taa zake ambazo zitakuwa ni sehemu ya matengenezo, siyo chini ya taa 200.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia, tuliwaomba mameneja wa mikoa walete mahitaji ya taa katika miji ambayo imekua. Kwa hiyo, nina uhakika kwamba, katika miji yote ambayo imekua itawekewa taa. Pia, tutapeleka taa 200 katika kila mkoa ambao wataamua taa zipi zimeharibika na wapi tuweze kuweka ili tuhakikishe miji yetu inapendeza, ukiwepo Mji wa Lushoto, kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge. Ahsante.

Name

Tumaini Bryceson Magessa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Primary Question

MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA aliuliza: - Je, lini TANROADS itamalizia kuweka taa za barabarani katikati ya Mji wa Korogwe, kwenye Barabara Kuu itokayo Dar es Salaam hadi Arusha?

Supplementary Question 3

MHE. TUMAINI B. MAGESSA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana. Ni lini Serikali itakamilisha uwekaji wa taa katika Mji Mdogo wa Katoro?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, tunaendelea kuweka taa katika Mji wa Katoro na tunakwenda sambamba kuongeza taa upande wa Buseresere. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge, tumepanga na tutaendelea kuziwekea taa katika mwaka huu, lakini tumepanga pia kuendelea kuweka taa pande zote, Buseresere na Katoro. Ahsante.