Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 35 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 451 2025-05-29

Name

Dr. Alfred James Kimea

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Korogwe Mjini

Primary Question

MHE. DKT. ALFRED J. KIMEA aliuliza: -

Je, lini TANROADS itamalizia kuweka taa za barabarani katikati ya Mji wa Korogwe, kwenye Barabara Kuu itokayo Dar es Salaam hadi Arusha?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, zoezi la uwekaji wa taa za barabarani ni endelevu. Hadi sasa jumla ya taa 89 zimewekwa Mji wa Korogwe kwenye urefu wa jumla ya kilometa 2.67. Kwa sehemu iliyobaki ya kilometa 2.0, uwekaji wa taa utaendelea kulingana na upatikanaji wa fedha. Ahsante.