Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Jesca Jonathani Msambatavangu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Iringa Mjini
Primary Question
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU K.n.y. MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza: - Je ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Chuo cha CBE katika Kata ya Lugalo – Kilolo?
Supplementary Question 1
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali ninaomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, nilitaka kujua pia katika huo mpango kabambe; je, mme-consider jiografia ya Wilaya ya Kilolo kwa kuwa pia jiografia yake ni kubwa na tungehitaji kwamba wanafunzi wote wanaolala katika hicho chuo wawe wa bweni?
Name
Exaud Silaoneka Kigahe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kaskazini
Answer
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana. Kwanza nichukue nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Justin Lazaro Nyamoga, kwani alipambania sana kuhakikisha Chuo cha CBE kinajengwa katika Mkoa wa Iringa na mahsusi Jimbo la Kilolo na tayari kama nilivyosema tumepata eneo pale na tulishakabidhiwa.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, ninamshukuru sana Mheshimiwa Jesca Msambatavangu ambaye Jimbo lake liko karibu sana na tunapojenga Chuo hiki cha CBE. Kwa hiyo, maana yake wananchi wa Jimbo la Iringa Mjini watafaidika sana kuliko hata Wanakilolo kwa maana ya jiografia.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa swali lake sasa ni kweli; moja ya mazingatio ambayo tumefanya ni kuhakikisha tunakuwa na mabweni kwa ajili ya wanachuo, kulala hapo ili kuhakikisha wanafunzi wote wanaendelea kusoma vizuri zaidi. Kwa kuwa Mkoa wa Iringa ni mkubwa na Nyanda za Juu Kusini, kwa hiyo, ni lazima kuwe na mabweni na miundombinu mingine stahiki ili waweze kusoma kwa usalama na kwa tija zaidi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved