Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 35 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 450 2025-05-29

Name

Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU K.n.y. MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza: -

Je ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Chuo cha CBE katika Kata ya Lugalo – Kilolo?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kilikabidhiwa eneo rasmi, Hati ya umiliki wa eneo la Chuo, Wilaya ya Kilolo mnamo tarehe 8 Julai, 2024 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia CBE inaandaa Mpango Kabambe (Master Plan) kwa ajili ya uendelezwaji wa kudumu wa Kampasi hiyo. Aidha, baada ya kukamilika kwa mpango kabambe, ujenzi wa Chuo kwa Kampasi ya Iringa iliyopo Kata ya Lugalo katika Wilaya ya Kilolo utaanza rasmi 2025/2026 kadri ya upatikanaji wa fedha.