Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Shally Josepha Raymond
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHALLY J. RAYMOND aliuliza: - Je, kuna walimu wangapi wa masomo ya hisabati na sayansi na kuna ziada au upungufu wa walimu wangapi katika shule za msingi na sekondari?
Supplementary Question 1
MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa upungufu ni mkubwa sana unaokaribia nusu, hadi sasa wanafunzi wengi wameelekea kuikataa sayansi, je, Serikali haioni kwamba jambo hilo ni la kufanyiwa ufumbuzi haraka?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kwa kuwa mabinti wengi au wanafunzi wengi wa kike wangependa sana kujifunza sayansi na shule zinaendelea kujengwa kila mkoa hasa za high school, lakini upungufu ndiyo kama ilivyoelezwa kwenye swali la msingi, je, ni athari gani ambazo zinaenda kutokea katika jambo hilo? (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nianze kwanza kumpongeza Mheshimiwa Shally Raymond ambaye amekuwa akifanya ufuatiliaji wa hali ya juu kuhusiana na masuala ya sekta ya elimu na hususan sekta hii ya elimu msingi na sekondari. Ninaomba nijibu maswali yake yote mawili kwa pamoja.
Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inafahamu kwamba kuna uhitaji wa kuendelea kupata walimu kwa ajili ya kufundisha wanafuzi wetu, na matokeo haya yote yanatokana na sababu ya msingi kabisa ya hatua ambazo zimechukuliwa na Serikali ya kutoa elimu bila malipo na udahili wa wanafunzi umeongezeka maradufu, na umetengeneza mazingira ambayo tunahitaji kupata walimu zaidi kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi wetu.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kuajiri walimu. Walimu wote, pia kwa kuzingatia uhitaji wa walimu wa masomo ya sayansi, katika Serikali ya Awamu ya Sita kwa kipindi hiki cha miaka minne walimu 45,742 tayari wameajiriwa na mpaka wakati huu tayari kimetoka kibali kingine cha kuendelea kuajiri walimu wengine zaidi ya 9,000. Miongoni mwa walimu hao wanaoajiriwa wapo Walimu wa Sayansi.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ya Awamu ya Sita inafanya uwekezaji mkubwa sana katika kuhakikisha inaweka kipaumbele katika masomo ya sayansi. Mheshimiwa Mbunge amesema kwamba anatambua jitihada ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kujenga shule za sayansi za bweni za wasichana kila Mkoa. Shule hizi zimepelekewa shilingi bilioni 4.45 kwa ajili ya kuhakikisha kwamba kunafanyika uwekezaji katika upande wa sayansi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, Serikali itaendelea na jitihada hizi zote kuhakikisha kwamba walimu wanapatikana wa wa masomo yote pia kwa kuzingatia uhitaji wa Walimu wa Sayansi watapatikana kwa ajili ya kuhakikisha kwamba, wanawafundisha watoto wetu na elimu inakuwa ni bora. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved