Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 35 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 446 | 2025-05-29 |
Name
Shally Josepha Raymond
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SHALLY J. RAYMOND aliuliza: -
Je, kuna walimu wangapi wa masomo ya hisabati na sayansi na kuna ziada au upungufu wa walimu wangapi katika shule za msingi na sekondari?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua changamoto ya upungufu wa walimu katika shule za msingi na sekondari. Serikali imekuwa ikiajiri walimu wa kada mbalimbali ikiwemo walimu wa masomo ya sayansi kadiri ya upatikanaji wa fedha.
Mheshimiwa Naibu Spika, mahitaji ya walimu wa masomo ya sayansi na hisabati ni 47,354, waliopo ni 30,044 na upungufu ni walimu 17,312. Aidha, mahitaji ya walimu kwa shule za msingi ni 298,687 waliopo ni 173,861 na upungufu ni 124,826.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kuajiri walimu wakiwemo walimu wa masomo ya sayansi kadri ya upatikanaji wa fedha.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved