Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 34 | Works and Transport | Wizara ya Uchukuzi | 407 | 2026-05-21 |
Name
Bazilio Kapunda Mbwilo
Sex
Male
Party
ACT
Constituent
Nkasi Kaskazini
Primary Question
MHE. BAZILIO K. MBWILO aliuliza:-
Je, lini Meli za Liemba na Mwongozo zitaanza tena kutoa huduma ndani ya Ziwa Tanganyika?
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Bazilio Kapunda Mbwilo, Mbunge wa Nkasi Kaskazini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Meli za MV Liemba na MV Mwongozo zitaanza kutoa huduma za usafiri katika Ziwa Tanganyika baada ya ukarabati kukamilika. Kwa sasa ukarabati wa MV Liemba unaendelea na upo katika hatua ya ufungwaji wa vifaa muhimu baada ya kupokelewa na inatarajiwa matengenezo hayo kukamilika mwezi Juni, 2026 na kukabidhiwa kwa TASHICO mwezi Julai, 2026, kwa ajili kuendelea kutoa huduma za usafirishaji ndani ya Ziwa Tanganyika. Aidha, taratibu za kuanza ukarabati mkubwa wa MV Mwongozo unaendelea kukamilishwa ili kuanza matengenezo hayo hivi karibuni.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved