Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 34 Public Service Management Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) 402 2026-05-21

Name

Stella Ikupa Alex

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y. MHE. STELLA I. ALEX aliuliza:-

Je, Serikali imefikia hatua gani katika kutekeleza Mwongozo wa Ajira na Mazingira ya Kazi kwa Watumishi wenye Ulemavu katika Taasisi za Umma?

Name

Regina Ndege Qwaray

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, ninaomba nijibu swali la Mheshimiwa Stella Ikupa Alex, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma, Toleo la Pili la Mwaka 2008, pamoja na Sheria ya Watu Wenye Ulemavu, Sura ya 183 imeweka masharti kuhusu Ajira na Mazingira ya Kazi kwa Watu wenye Ulemavu katika Utumishi wa Umma na Sekta Binafsi. Aidha, katika kutekeleza Masharti hayo katika Taasisi za Umma kwa Watumishi wenye Ulemavu, Serikali imepiga hatua mbalimbali zikiwemo:-

(i) Kutunga Kanuni za Utumishi wa Umma za Mwaka, 2022;

(ii) Kutunga Kanuni za Uendeshaji wa Shughuli za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma za Mwaka, 2021; na

(iii) Kuandaa Mwongozo wa Huduma kwa Watumishi wa Umma wenye Ulemavu wa Mwaka, 2008;

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuweka misingi thabiti ya utekelezaji wa Sera, Sheria na Miongozo kuhusu Watumishi wenye ulemavu kwa kutoa elimu, kuhamasisha na kusimamia ujenzi wa miundombinu fikivu na rafiki kwa watu wenye ulemavu katika Utumishi wa Umma ili kuhakikisha mazingira ya kazi yanakuwa salama na wezeshi, ahsante. (Makofi)