Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 29 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 337 2026-05-14

Name

Salehe Mbwana Mhando

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Primary Question

MHE. SALEHE M. MHANDO aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga madaraja yaliyoharibika katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Kilindi ili kurahisisha usafiri?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Salehe Mbwana Mhando, Mbunge wa Jimbo la Kilindi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wilaya ya Kilindi ina mtandao wa barabara wenye urefu wa kilometa 871.59 unaohudumiwa na TARURA. Aidha, ina jumla ya vivuko 1,066 ambapo madaraja makubwa ni matatu, box kalvati 592, Solid drift 466, vented drift tano. Daraja moja linafanya kazi na yaliyoharibika mawili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kufanya usanifu na kujenga madaraja ambapo mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali ilitenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Mgera lenye upana wa meta 20 kwa awamu ya kwanza na ujenzi umefikia 60%.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, kwa mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Daraja hilo la Mgera. Aidha, Serikali imeshakamilisha usanifu wa Daraja la Negero lenye upana wa meta 80 ambapo ujenzi wake unakadiriwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.72.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Serikali inaendelea na ukarabati wa madaraja yaliyochakaa katika Wilaya ya Kilindi ambapo katika mwaka wa fedha 2023/2024 ilikarabati Daraja la Ngeze, Barabara ya Kwekivu - Ngeze kwa gharama ya shilingi milioni 7.8 na kujenga box kalvati jipya Barabara ya Mapanga - Mlingotini kwa gharama ya shilingi milioni 24.14.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga bajeti ili kuendelea na ujenzi wa madaraja mapya na kukarabati madaraja yaliyochakaa kote nchini ikiwemo Jimbo la Kilindi.