Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 24 Justice and Constitutional Affairs Wizara ya Katiba na Sheria 276 2026-05-07

Name

Zacharia Paulo Issaay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Mjini

Primary Question

MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza: -
Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Mbulu ambao umesimama kwa muda mrefu?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania imeendelea kutekeleza Mpango wa Ujenzi na Ukarabati wa majengo ya Mahakama kwa lengo la kuimarisha miundombinu ya utoaji haki katika ngazi mbalimbali. Mpango huu unahusisha ujenzi wa majengo mapya pamoja na ukarabati wa majengo yaliyopo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika utekelezaji wa mpango huo, ujenzi wa jengo la Mahakama ya Wilaya ya Mbulu ulianza katika mwaka wa fedha 2024/2025. Hata hivyo, mradi huo umechelewa kukamilika kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa utekelezaji wake. Tayari changamoto hizo zimetatuliwa na ujenzi wa jengo hilo unaendelea na unatarajiwa kukamilika ifikapo Novemba, 2026.