Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 11 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 127 2026-04-17

Name

Naomy Duncan Mwaipopo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NAOMY D. MWAIPOPO aliuliza: -

Je, Serikali ina mikakati gani ya kutatua Migogoro ya Ardhi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji?

Name

Kaspar Kaspar Mmuya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ruangwa

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, sasa naomba kujibu swali la Mheshimiwa Naomy Duncan Mwaipopo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu wa utatuzi wa migogoro ya ardhi unasimamiwa na Sheria ya Mahakama za Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi, Sura ya 216. Sambamba na Sheria hii, Wizara imeendelea kutatua migogoro hiyo kiutawala. Manispaa ya Kigoma Ujiji ni miongoni mwa maeneo yenye migogoro ya ardhi inayotokana na aina ya vyanzo mbalimbali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa kanzidata iliyopo, jumla ya migogoro ya ardhi 1,092 ilipokelewa na kusajiliwa katika Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo kati ya hiyo, migogoro 1,046 imetatuliwa kiutawala na migogoro 46 ipo kwenye hatua mbalimbali za utatuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kushughulikia migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Manispaa ya Kigoma Ujiji, Serikali imeendelea kuweka mikakati inayolenga kuhakikisha migogoro hiyo inapungua na hatimaye kumalizika kabisa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mikakati hiyo ni pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya ardhi ili kuwaepusha wananchi kujiingiza katika migogoro ya ardhi inayoweza kuzuilika, kuwakumbusha watumishi kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu pamoja na kusimamia nidhamu kwa watumishi wa Sekta ya Ardhi ili waweze kutekeleza majukumu kwa kuzingatia maadili ya taaluma zao na pia kuendeleza Programu ya Kliniki za Ardhi ambapo wananchi wenye migogoro wameendelea kupata fursa ya kukutana na wataalamu na viongozi moja kwa moja na kutatuliwa kero zao.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kuwasilisha.