Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 24 Natural Resources and Tourism Wizara ya Maliasili na Utalii 273 2026-05-07

Name

Kangi Alphaxard Lugola

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Primary Question

MHE. KANGI A. LUGOLA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti kero ya mamba wanaodhuru wananchi katika Jimbo la Mwibara?

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Kangi Alphaxard Lugola, Mbunge wa Jimbo la Mwibara, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imechukua hatua mbalimbali za kudhibiti mamba katika Jimbo la Mwibara ambapo katika mwaka wa fedha 2024/2025, Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia TAWA ilijenga jumla ya vizimba vinne vya kuzuia mamba katika vijiji vya Buzimbwe, Kasahunga, Nampangala na Nyarugoma.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Wizara inaendelea na ujenzi wa vizimba viwili katika vijiji vya Nyamitwebili na Namibu. Aidha, kwa kuwa changamoto hii haiwezi kwisha kwa mara moja, Wizara kupitia Taasisi ya TAWA itaendelea kujenga vizimba kwenye maeneo yenye changamoto za mamba kudhuru watu kwenye Ziwa Victoria katika Wilaya za Jimbo la Mwibara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, Wizara imekuwa ikitoa elimu kwa wananchi wa Jimbo la Mwibara ambapo kati ya Mwezi Julai, 2025 hadi Machi, 2026, jumla ya mikutano 12 ilifanyika. Katika mikutano hiyo, wananchi 3,665 ikijumuisha watu wazima 904 na wanafunzi 2,761 walipatiwa elimu ya namna bora ya kutumia vizimba na kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na mamba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, ili kuongeza wigo wa kutoa elimu kwa wananchi, Wizara ilitoa elimu kwa njia ya redio na televisheni ambapo jumla ya vipindi vitano vya redio na televisheni vitatu vilitolewa. Vipindi hivyo, vilitolewa katika redio za Bunda FM na Redio Mazingira, na televisheni ya Star TV ambazo zinasikika zaidi katika Kanda ya Ziwa ikiwemo Jimbo la Mwibara.