Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 24 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 270 | 2026-05-07 |
Name
Onesmo Merdson Mnkondya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbozi
Primary Question
MHE. ONESMO M. MNKONDYA aliuliza: -
Je, lini Serikali itajenga chuo kikuu katika Mkoa wa Songwe?
Name
Wanu Hafidh Ameir
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Onesmo Merdson Mnkondya, Mbunge wa Mbozi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuongeza fursa za upatikanaji wa Elimu ya Juu na kuchochea maendeleo ya kiuchumi, Serikali inaendelea na kukamilisha ujenzi wa kampasi za taasisi za elimu ya juu katika maeneo mbalimbali nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Songwe una taasisi za Elimu ya Juu ikiwemo Kampasi ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) ambayo kupitia mradi wa Technical Education Labour Market Survey, Serikali inafanya upanuzi wa miundombinu. Upanuzi huu unahusisha ujenzi wa jengo la ghorofa nne la taaluma ambalo litakuwa na madarasa, maabara pamoja na karakana. Lengo ni kuongeza udahili wa wanafunzi katika fani mbalimbali kuanzia ngazi ya cheti hadi degree.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved