Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 11 | Works and Transport | Wizara ya Ujenzi | 125 | 2026-04-17 |
Name
Kunti Yusuph Majala
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. KUNTI Y. MAJALA aliuliza: -
Je, lini ujenzi wa barabara kutoka Handeni kupitia Olboloti - Mrijo - Chemba - Kwamtoro hadi Singida utaanza?
Name
Abdallah Hamis Ulega
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkuranga
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI K.n.y. WAZIRI WA UJENZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Kunti Yusuph Majala kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeanza ujenzi wa Barabara ya Handeni – Kibirashi – Kiteto – Mrijo – Chemba hadi Singida yenye urefu wa kilometa 424.24 kwa awamu, ambapo kwa sehemu ya kwanza ya kutoka Handeni – Mafuleta (kilometa 20) ujenzi umefikia 52.6%.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, sehemu ya pili ya Mafuleta – Kileguru (kilometa 30) na Kibaya – Kisima (kilometa 50) wakandarasi wapo kwenye maandalizi ya kuanza ujenzi. Kwa sehemu iliyobaki, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) wako kwenye majadiliano ya awali ya kuijenga kwa utaratibu wa PPP.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved