Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 6 | Health and Social Welfare | Wizara ya Afya | 59 | 2026-04-10 |
Name
Eric James Shigongo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Buchosa
Primary Question
MHE. JOHN F. NZILANYINGI K.n.y. MHE. ERICK J. SHIGONGO aliuliza: -
Je, lini Serikali itatoa chanjo ya homa ya ini kwa Watanzania wote?
Name
Dr. Florence George Samizi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Muhambwe
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Afya, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Eric James Shigongo, Mbunge wa Buchosa, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwa sasa, chanjo ya ugonjwa wa homa ya ini inatolewa nchini kama sehemu ya ratiba ya chanjo za watoto wachanga, ambapo mtoto hupatiwa chanjo hiyo muda mfupi baada ya kuzaliwa, pamoja na kutolewa kwa makundi maalum yaliyo katika hatari zaidi, wakiwemo watoa huduma za afya na makundi mengine yenye uwezekano mkubwa wa kuambukizwa.
Mheshimiwa Spika, aidha, Chanjo ya Homa ya Ini inatolewa katika Hospitali za Taifa, kanda, mikoa na hospitali zote za wilaya na halmashauri, ambapo mwananchi anaweza kupata chanjo hiyo baada ya kupimwa na ikibainika hana virusi vya Homa ya Ini aina B hupewa chanjo hiyo ambayo hutolewa kwa dozi tatu kwa vipindi tofauti.
Mheshimiwa Spika, Wizara imeunda timu ya wataalamu kwa ajili ya kuandaa andiko litakalotoa mwelekeo na maoteo ya gharama zinazohitajika kutekeleza lengo la kutoa huduma ya Chanjo ya Homa ya Ini kwa Watanzania wote. Mara litakapokamilika hatua za utekelezaji wa maoni ya maandiko hayo yataweza kufanyiwa kazi.
Mheshimiwa Sika, ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved