Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 6 | Home Affairs | Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi | 55 | 2026-04-10 |
Name
Kija Limbu Ntemi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Katoro
Primary Question
MHE. KIJA L. NTEMI aliuliza: -
Je, lini Serikali itatoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Zimamoto ili kusaidia majanga ya moto yanapotokea Katoro?
Name
Kaspar Kaspar Mmuya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ruangwa
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali Na. 55 la Mheshimiwa Injinia Kija Limbu Ntemi, Mbunge wa Katoro, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na jitihada za kusogeza huduma za zimamoto na uokoaji karibu na wananchi ikiwemo ujenzi wa vituo vya zimamoto na uokoaji. Aidha, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limepata kiwanja Na. 1384 kilichopo Kitalu Namba “A” chenye ukubwa wa mita za mraba 4,987 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Zimamoto na Uokoaji katika Mji wa Katoro, na utaratibu wa kupata hatimiliki zinaendelea.
Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved