Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 6 Works, Transport and Communication Wizara ya Uchukuzi 52 2026-04-10

Name

Mwanaisha Ng'anzi Ulenge

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE aliuliza: -

Je, lini Serikali itatwaa maeneo ya karibu na Bandari ya Tanga, ili kuongeza eneo la utekelezaji wa shughuli za Bandari?

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi, Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa Mnyaa, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Engineer Ulenge, Mbunge wa Viti Maalumu, Mkoa wa Tanga, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa eneo katika Bandari ya Tanga, Serikali kupitia TPA, inaendelea na taratibu za utwaaji wa eneo karibu na Lango Namba Mbili na eneo la Police Marine, ili yatumike kwa ajili ya shughuli za kibandari.

Mheshimiwa Spika, pamoja na utwaaji wa maeneo hayo, TPA inaendelea na mpango wa matumizi bora ya maeneo yaliyopo ndani ya bandari, ikiwa ni pamoja na uhamishaji wa baadhi ya maghala, ili kuongeza maeneo ya kufanyia shughuli za kibandari.