Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 6 Water and Irrigation Wizara ya Maji 50 2026-04-10

Name

Zuena Athumani Bushiri

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZUENA A. BUSHIRI aliuliza:-

Je, Serikali ina mkakati gani wa kujenga chanzo cha maji kilichobebwa na mafuriko katika Kata ya Maore Same Mashariki?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maji, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Zuena Athumani Bushiri, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, katika mpango wa muda mfupi, Serikali kwa kushirikiana na wananchi wa Kata ya Maore imekamilisha ukarabati wa dharura wa chanzo cha maji Maore na sasa zaidi ya wananchi 14,000 wa vijiji vitatu vya Maore, Kadandu na Mheza vinavyopatikana katika kata hiyo, wanapata huduma ya majisafi na salama.

Mheshimiwa Spika, katika mpango wa muda mrefu, Serikali inaendelea na usanifu wa mradi utakaojumuisha pia maboresho ya ujenzi wa chanzo cha Maore. Usanifu wa mradi huo unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2025/2026 na utekelezaji wake kufanyika baada ya fedha kupatikana.