Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 6 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 48 2026-04-10

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. FESTO R. SANGA aliuliza:-

Je, lini Serikali itaongeza bajeti ya ujenzi na ukarabati wa barabara za TARURA za Wilaya ya Makete zenye urefu wa Km. 680.3 kutoka shilingi bilioni 3.2 hadi shilingi bilioni saba?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Festo Richard Sanga, Mbunge wa Jimbo la Makete kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kutambua umuhimu wa barabara za vijijini na mijini kwa kutoa huduma za usafirishaji na usafiri kwa wananchi, imeendelea kuongeza bajeti za ujenzi na ukarabati kwa wilaya zote nchini ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Makete.

Mheshimiwa Spika, katika Wilaya ya Makete, Serikali imeendelea kuongeza bajeti ya fedha za ujenzi na ukarabati na ukarabati wa barabara kutoka shilingi milioni 834.59 katika mwaka wa fedha 2020/2021 hadi kufikia shilingi bilioni 3.9 katika mwaka wa fedha 2024/2025.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuboresha bajeti ya barabara za vijijini na mijini kote nchini zikiwemo barabara za Wilaya ya Makete.