Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 6 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 47 | 2026-04-10 |
Name
Emanuel Qambaji Nuwas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Vijijini
Primary Question
MHE. DKT. EMANUEL Q. NUWAS aliuliza: -
Je, Serikali haioni haja ya kuongeza muda wa marejesho ya Mikopo ya asilimia mbili kwa Watu wenye Ulemavu ili kujenga usawa?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Mwongozo wa utoaji, usimamizi na urejeshaji wa fedha za mikopo ya 10% kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, hakuna ukomo au muda maalum wa marejesho uliowekwa.
Mheshimiwa Spika, muda na utaratibu wa marejesho kwa makundi yote ikiwemo kundi la watu wenye ulemavu hufuata makubaliano kati ya halmashauri na wakopaji kwa kuzingatia aina ya miradi na aina ya mtiririko wa fedha katika shughuli iliyoombewa mkopo ili kuongeza ufanisi wa shughuli za wajasiriamali na marejesho ya mikopo.
Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kusimamia Sheria, Kanuni na Miongozo ili kuwezesha makundi haya kunufaika na fursa hizi za mikopo ya 10%, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved