Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 9 Natural Resources and Tourism Wizara ya Maliasili na Utalii 102 2026-04-15

Name

Ester Amos Bulaya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTER A. BULAYA aliuliza: -

Je, lini ujenzi wa Makao Makuu ya TANAPA Kanda ya Magharibi utaanza?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maliasili na Utalii, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Ester Amos Bulaya, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) linasimamia Hifadhi za Taifa 21 zilizogawanywa katika Kanda Nne, ikiwemo Kanda ya Magharibi, ambayo Makao Makuu yake yapo Mji wa Bunda, Mkoa wa Mara. Kanda hii inajumuisha Hifadhi za Taifa zipatazo tisa zinazosimamiwa na TANAPA, ikiwemo Hifadhi za Taifa Serengeti, Visiwa vya Saanane na Rubondo, Burigi - Chato, Milima Mahale, Ibanda - Kyerwa, Rumanyika - Karagwe, Mto Ugalla na Gombe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Serikali imetenga eneo lenye ukubwa wa ekari 41.13 katika eneo la Kata ya Balili, Bunda Mjini, kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Kanda ya Magharibi ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2026/2027, Wizara kupitia TANAPA imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1.8 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hizo. Aidha, taratibu zote za maandalizi za kuanza ujenzi wa mradi huo, ikiwemo usanifu wa majengo na gharama za ujenzi wa mradi huo, zimekamilika. Ahsante sana.