Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 9 | Health and Social Welfare | Wizara ya Afya | 101 | 2026-04-15 |
Name
Mariam Anzuruni Mungula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MARIAM A. MUNGULA aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa elimu kwa wanawake juu ya magonjwa ya tezi ya shingo (thyroid) na yanayosababisha ukomo wa hedhi?
Name
Dr. Florence George Samizi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Muhambwe
Answer
NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Afya ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Mariam Anzuruni Mungula, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ugonjwa wa tezi ya shingo ni miongoni mwa magonjwa yasiyoambukiza, ambapo wanawake wana hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu kuliko wanaume. Tafiti zinaonesha wagonjwa tisa kati ya kumi ni wanawake. Aidha, wanawake 12 kati ya 100 wana hatari ya kupata ugonjwa huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, visababishi vya ugonjwa huo ni tezi ya shingo kushambuliwa na kinga ya mwili (autoimmune), kupanda na kushuka kwa homoni (estrogene, progestrone, thyroid) katika mazingira ya upungufu wa madini joto mwilini, kusababishwa na familia, umri zaidi ya miaka 60, msongo wa mawazo na namna ya maisha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na mpango wa utoaji elimu kwa wanawake juu ya magonjwa ya tezi ya shingo kwa kufanya yafuatayo: -
(1) Kutoa elimu kwa jamii kupitia vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo redio, runinga, mitandao ya kijamii, mabango na vipeperushi kuhusu chanzo dalili na kinga ya ugonjwa huu;
(2) Kuendelea kusimamia na kuhakikisha chumvi yote inayozalishwa na kuuzwa nchini inakuwa na kiwango stahiki cha madini joto;
(3) Serikali inaimarisha kampeni jumuishi za lishe kwa kuendelea kuhamasisha matumizi sahihi ya vyakula vyenye madini joto na lishe bora;
(4) Serikali imeendelea kutoa elimu na kuhamasisha jamii kutumia vyakula vyenye madini joto ikiwemo, chumvi yenye madini joto pamoja na vyakula vyenye madini joto;
(5) Kuimarisha na kupanua wigo wa uchunguzi, upatikanaji wa vipimo na huduma za matibabu ya magonjwa ya tezi katika ngazi zote za huduma za afya; na
(6) Kuwajengea uwezo watoa huduma za afya, ili waweze kutambua mapema na kutoa huduma sahihi kwa wagonjwa wa tezi ya shingo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved