Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 26 Water and Irrigation Wizara ya Maji 334 2025-05-16

Name

Anatropia Lwehikila Theonest

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTHER N. MATIKO K.n.y. MHE ANATROPIA L. THEONEST aliuliza:-

Je, ni miradi gani ya maji inatekelezwa Kyerwa, mkandarasi ni nani, inagharimu kiasi gani na lini itakamilika?

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI K.n.y. WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imekamilisha utekelezaji wa miradi miwili ya Nyamiaga-Nyakatera na Mabira kwa gharama ya shilingi 2,159,974,805.35 iliyopo Wilayani Kyerwa, Mkoa wa Kagera. Miradi hiyo imetekelezwa na wakandarasi wa ndani wa Kampuni za JAMTA Investment na AMRI AMIRI Co. Ltd. ambapo kwa sasa inanufaisha zaidi ya wakazi 26,123 waishio katika vijiji saba vya Masheshe, Nyamiaga, Kagu, Nyakatera, Mabira, Nyakatete na Omkagando.

Mheshimiwa Spika, vilevile Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi minne ya Runyinya - Chanya, Kaisho - Isingiro, Kimuli – Rwanyango - Chakalisa na Kikukuru - Rubirizi kupitia wakandarasi wa Makampuni ya JAMTA, SERENGETI na OTONDE kwa jumla ya gharama ya shilingi zaidi ya bilioni 13. Miradi hiyo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji na inatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2025.

Mheshimiwa Spika, aidha, Serikali imekamilisha uchimbaji wa visima vitano vya Jimbo la Kyerwa katika Vijiji vya Nyakatuntu, Nyakakoni, Songambele, Kamuli na Nyaruzumbura kupitia programu maalum ya uchimbaji wa visima 900. Kwa sasa kazi inayoendelea ni ufungaji wa pampu na ujenzi wa miundombinu rahisi ya kutolea huduma kwa wananchi inayotarajiwa kukamilika ndani ya mwezi Mei, 2025.