Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 4 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 24 | 2026-04-08 |
Name
Saashisha Elinikyo Mafuwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hai
Primary Question
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha Afya Mnadani?
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Saashisha Elinikyo Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 hadi 2025/2026, Serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 3.08 kwa ajili ya ujenzi wa ukarabati wa miundombinu katika Hospitali ya Wilaya ya Hai, ujenzi wa Vituo vya Afya Chekimaji, Masama na Nkwansira pamoja na ukamilishaji wa maboma nane ya zahanati katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali imetoa shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kimkakati cha KIA. Ujenzi wa kituo hicho umekamilika na taratibu za usajili zinaendelea na kitaanza kutoa huduma za wagonjwa wa nje (OPD) mwezi Mei mwaka huu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa awamu kwa ajili ujenzi wa vituo vya afya kote nchini kikiwemo Kituo cha Afya Mnadani katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved