Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 2 Sitting 6 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 105 2026-02-03

Name

Margaret Simwanza Sitta

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Urambo

Primary Question

MHE. JAPHAEL M. LUFUNGIJA K.n.y. MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza: -

Je, kwa nini Mkulima analazimika kununua mbegu za mahindi kila mwaka badala ya kutumia zile ambazo amevuna?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkulima hulazimika kununua mbegu kila msimu ili aweze kupata tija iliyodhamiriwa kwa sababu mbegu anazonunua katika maduka ya pembejeo huwa zimepitia majaribio ya kisayansi katika maabara ili kuthibitisha ubora wa sifa mbalimbali, ikiwemo kiwango cha uzalishaji, uhimilivu wa magonjwa na ukame. Mkulima anapovuna mazao na kutumia kama mbegu kwa mara ya pili au zaidi husababisha sifa za mwanzo za mbegu husika kupungua ama kupotea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, asilimia kubwa ya mbegu zinazotumiwa na wakulima nchini, ni mbegu aina ya chotara ambazo utengenezaji ama uzalishaji wake hutumia aina mbili au zaidi tofauti za mbegu wazazi kutoka jamii moja. Kutokana na sababu hiyo, iwapo mbegu hizo zitatumika kama mbegu kwa mara ya pili au zaidi husababisha kupotea au kupungua kwa sifa bora za mbegu hivyo kuchangia kushuka kwa tija na uzalishaji wa mazao ya mkulima.