Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 2 Sitting 6 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 104 2026-02-03

Name

Suma Ikenda Fyandomo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SUMA I. FYANDOMO aliuliza: -

Je, lini Kiwanda cha Chai cha WATCO kilichopo Katumba – Tukuyu Wilaya ya Rungwe, kitafunguliwa?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara imefanya jitihada za kuhakikisha Kiwanda cha Chai cha WATCO kinafunguliwa ambapo Kampuni ya WATCO inayosimamia kiwanda hicho imepata mkopo ambao umetumika kulipa madai ya wakulima, wafanyakazi na watoa huduma wengine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya malipo hayo, hatua inayofuata ni ufunguzi wa kiwanda hicho ambacho kinatarajiwa kufunguliwa ifikapo tarehe 2 Machi, 2026 baada ya kukamilika kwa usafi na ukarabati. (Makofi)