Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 2 Sitting 6 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 102 2026-02-03

Name

Dr. Jasson Samson Rweikiza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Vijijini

Primary Question

MHE. DKT. JASSON S. RWEIKIZA aliuliza: -

Je, lini wananchi wa Bukoba watawezeshwa kwa kupewa vizimba vingi zaidi vya samaki ili kushiriki katika kukuza uchumi?

Name

Ng'wasi Damas Kamani

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ninaomba sasa kujibu swali la Mheshimiwa Jasson Samson Rweikiza, Mbunge wa Bukoba Vijijini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) inaendelea na zoezi la utoaji wa mikopo ya masharti nafuu ya vizimba, vifaranga na chakula cha samaki. Katika awamu ya kwanza mikopo ya vizimba 44, Bukoba 30, Muleba 12, Misenyi viwili yenye thamani ya shilingi milioni 986.80 ilitolewa Mkoani Kagera kwa wanufaika 101.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2025/2026, Wizara imepokea kiasi cha shilingi bilioni saba kutoka Hazina kwa ajili ya kuwezesha vijana kupata mitaji kupitia mikopo yenye masharti nafuu. Fedha hizo zitatumika kukopesha vijana 308 waliohitimu mafunzo hayo wakiwemo vijana 32 kutoka Mkoa wa Kagera.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, Wizara inatarajia kupokea sehemu ya shilingi bilioni 200 ambazo ni ahadi ya Mheshimiwa Rais ndani ya siku 100, zitazotekelezwa katika kuwezesha mikopo ya vizimba. Aidha, Wizara inaendelea kutafuta vyanzo vingine vya fedha ili kuendelea kutoa mikopo ya vizimba katika maeneo mbalimbali hapa nchini wakiwemo vijana wa Bukoba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kutoa rai kwa Halmashauri kuelekeza sehemu ya mikopo ya 10% katika ufugaji samaki kwa vizimba iwapo zina maeneo yanayofaa kwa shughuli hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kuwasilisha.