Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 2 | Sitting 6 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 92 | 2026-02-03 |
Name
Jackson Gedion Kiswaga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalenga
Primary Question
MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y. MHE. JACKSON G. KISWAGA aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa kipande cha barabara kutoka Tosamaganga hadi Igwachanya kwa kiwango cha lami?
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Jackson Gedion Kiswaga, Mbunge wa Kalenga, ambalo limeulizwa na Mbunge wa Temeke, Mheshimiwa Mariam Kisangi kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Tosamaganga – Igwachanya ni moja kati ya barabara muhimu inayounganisha barabara kuu ya TANZAM na barabara ya Mkoa ya Iringa hadi Msembe yenye urefu wa kilometa 11. Mpaka sasa jumla ya kilometa 10.1 zimeshajengwa kwa kiwango cha lami na kilometa 0.9 iliyosalia inatarajia kujengwa katika mwaka 2025/2026 kupitia Wizara ya Ujenzi chini ya usimamizi wa TANROADS.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, mkandarasi atakayetekeleza kazi hiyo ni Plan Engineering Company na mradi utatekelezwa kwa gharama ya shilingi milioni 829.88.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved