Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 2 Sitting 6 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 90 2026-02-03

Name

Eng. Ezra John Chiwelesa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Biharamulo Magharibi

Primary Question

MHE. ENG. EZRA J. CHIWELESA aliuliza: -

Je, lini Serikali itatimiza ahadi yake ya kupeleka gari la kubebea wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Nyakahura Wilayani Biharamulo?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Engineer Ezra John Chiwelesa, Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali katika kipindi cha mwaka 2021/2022 hadi 2024/2025 imenunua jumla ya magari 594 zikiwemo ambulance 382 na magari ya usimamizi ufuatiliaji 212 katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kote nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo imepokea gari moja la kubebea wagonjwa mwezi Novemba, 2023 na kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Biharamulo. Aidha, idadi hii inafanya Halmashauri ya Biharamulo kuwa na jumla ya magari matatu ya kubebea wagonjwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa magari ya wagonjwa kwa awamu kwa ajili ya vituo vya afya vyenye uhitaji kote nchini kikiwemo Kituo cha Afya Nyakahura. (Makofi)