Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 2 | Sitting 2 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 24 | 2026-01-28 |
Name
Chacha Mwita Wambura
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Geita Mjini
Primary Question
MHE. ENG. CHACHA M. WAMBURA aliuliza:-
Je, hatua gani zimefikiwa katika kuandaa mpango wa kuendeleza na kukamilisha ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu - Manispaa ya Geita?
Name
Dr. Jafar Rajab Seif
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF): alijibu:-
Mheshimiwa Spika, uwanja wa mpira wa miguu - Geita ulianza kujengwa mwaka 2021 kwa kutumia fedha za uwajibikaji wa kijamii wa mashirika (CSR) kwa gharama ya shilingi bilioni 5.46 kupitia mgodi wa Geita Gold Mine. Hata hivyo, ujenzi ulisimama mwaka 2023 ukiwa 71%, baada ya Mkandarasi EFQ Co. Ltd kusitishiwa mkataba kutokana na mabadiliko ya kanuni ya miradi ya CSR.
Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na mgodi wa Geita Mine Ltd imepata mkandarasi mshauri NORPLAN ambaye amefanya mapitio ya gharama halisi za kukamilisha ujenzi wa uwanja huo na kiasi cha shilingi bilioni tano zinahitajika. Aidha, Serikali inaendelea na mapitio ya gharama zilizowasilishwa na mkandarasi mshauri ili kuweza kuendelea na ujenzi kupitia fedha za CSR zitakazotengwa katika mwaka 2026/2027.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved