Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 2 Sitting 2 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) 23 2026-01-28

Name

George Natany Malima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Primary Question

MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza:-

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa kituo cha afya Kata ya Iwondo ili wananchi waanze kupata huduma?

Name

Dr. Jafar Rajab Seif

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. JAFAR R. SEIF) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa George Natany Malima, Mbunge wa Jimbo la Mpwapwa, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu.

Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2021 mpaka 2022 Serikali ilitoa shilingi milioni 500, kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Iwondo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa. Fedha hizo zilitumika kujenga Jengo la Huduma za Wagonjwa wa Ne (OPD), maabara na kichomea taka, ambayo yamekamilika na yanatumika. Jengo la huduma za uzazi na upasuaji, ujenzi upo hatua ya plasta na jengo la kufulia hatua ya kupaka rangi.

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa imetenga jumla ya shilingi milioni 50 katika mwaka wa fedha 2025/2026. Mwaka 2026/2027 itatenga jumla ya shilingi milioni 50, kwa ajili ya kukamilisha majengo yaliyosalia katika Kituo cha Afya Iwondo. (Makofi)