Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 2 | Sitting 2 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 22 | 2026-01-28 |
Name
Dr. Yahaya Esmail Nawanda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyumbu
Primary Question
MHE. DKT. YAHYA E. NAWANDA aliuliza:-
Je, lini Stendi ya Mabasi ya Mji wa Kitangari, Newala, itajengwa?
Name
Kwagilwa Reuben Nhamanilo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Handeni Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO) alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Yahya Esmail Nawanda, Mbunge wa Newala Vijijini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Newala ina stendi ya mabasi iliyopo katika Mji wa Kitangari, ambayo imepangwa kutengewa fedha katika Mpango wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 kupitia mapato ya ndani ya halmashauri. Kutokana na stendi hiyo kutokidhi mahitaji ya sasa ya usafiri, halmashauri imepanga kufanya maboresho ya awali kwa kiwango cha changarawe ili kuboresha utoaji wa huduma za wananchi.
Mheshimiwa Spika, sambamba na maboresho hayo halmashauri imeanza kutafuta eneo mahsusi, kwa ajili ya ujenzi wa stendi ya kisasa itakayokidhi mahitaji ya Mji wa Kitangari na maeneo ya jirani.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved