Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 8 | Water and Irrigation | Wizara ya Maji | 80 | 2026-04-14 |
Name
Boniventura Destery Kiswaga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Magu
Primary Question
MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA aliuliza: -
Je, lini Serikali itatoa fedha za kumalizia Mradi wa Maji Lugeye Kigangama uliosimama kwa miaka miwili sasa?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Boniventura Kiswaga, Mbunge wa Jimbo la Magu, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kipaumbele cha Serikali ni kuhakikisha miradi yote inayoendelea na utekelezaji, inakamilika na kuanza kutoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi ukiwemo mradi wa Lugeye – Kigangama uliopo Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza.
Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huo unagharimu zaidi ya shilingi bilioni saba na umefikia wastani wa 65% za utekelezaji ambapo unahusisha ujenzi wa dakio (intake) yenye uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 3.7 kwa siku kutoka chanzo cha ziwa Victoria. Ujenzi wa mtambo wa kutibu maji (treatment plant), ujenzi wa tanki lenye ujazo wa lita 1,000,000, ulazaji wa mabomba umbali wa kilometa 52 sanjari na ujenzi wa vituo 10 vya kuchotea maji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kupeleka fedha za utekelezaji wa mradi huo kadiri zinavyopatikana ili kuhakikisha unakamilika ndani ya mwaka wa fedha 2026/2027 na kuanza kutoa huduma iliyokusudiwa kwa zaidi ya wananchi 47,076 waishio katika vijiji saba vya Kitongosima, Lugeye, Kigangama, Bundilya, Nyanguge, Bugumangala na Muda.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved