Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 8 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 76 | 2026-04-14 |
Name
Dr. Selemani Said Jafo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kisarawe
Primary Question
MHE. DKT. SELEMANI S. JAFO aliuliza: -
Je, lini Serikali itatenga fedha za ujenzi wa shule ya sekondari eneo la Mafizi ili kupunguza umbali kwa wanafunzi wa Mafizi na Nyani?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Selemani Saidi Jafo, Mbunge wa Jimbo la Kisarawe, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kujenga shule za sekondari katika kata ili kuwapunguzia umbali wanafunzi kote nchini, ikiwemo katika Wilaya ya Kisarawe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 hadi 2023/2024, Serikali imejenga shule mpya tano za sekondari, ikiwemo shule ya Dkt. Selemani Jafo, Kitanga Kisarawe, Muungano Boga, Visiga na Vitende katika Halmashauri ya Kisarawe kwa gharama ya shilingi bilioni 1.83.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wanafunzi wanaotoka Mafizi na Nyani wanasoma katika Shule ya Sekondari Gwata Kisarawe, Kata ya Mafizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuwaondolea changamoto ya umbali kwa wanafunzi, Serikali katika mwaka wa fedha 2025/2026 imepeleka shilingi milioni 68.81 kwa ajili ya ukamilishaji wa bweni ambapo kwa sasa liko hatua ya umaliziaji.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved