Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 7 | Community Development, Gender and Children | Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum | 68 | 2026-04-13 |
Name
Mariam Madalu Nyoka
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MARYAM AZAN MWINYI K.n.y. MHE. MARIAM M. NYOKA aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kuimarisha vikundi vya wanawake kiuchumi katika Mkoa wa Ruvuma ili wapate fursa za masoko, mafunzo na mitaji?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Mariam Nyoka, Mbunge wa Viti Maalum.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inashirikiana na wadau kutekeleza mikakati ya kuendeleza vikundi vya wanawake kiuchumi kwenye mikoa yote, ambapo kwa Mkoa wa Ruvuma jumla ya vikundi vya kiuchumi 9,430 vya wanawake vimeshasajiliwa na usajili unaendelea. Baada ya usajili wa vikundi hivyo, mikakati ifuatayo inaendelea ili kuiimarisha viweze kukidhi kupata mitaji:-
(i) Kutoa elimu na mafunzo ya ujasiriamali ili vikundi viwe na uwezo wa kujiendesha na kutekeleza miradi yenye uendelevu inayokuza ajira na kuongeza kipato;
(ii) Kutoa elimu ya mikopo ikiwemo ile isiyo na riba kuanzia iliyopo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa na kwenye Taasisi za umma na binafsi;
(iii) Kuendelea kurasimisha biashara za wanawake ambapo kupitia mkakati huu, vikundi vinaendelea kuelimishwa na kusajili biashara zao ili zitambulike kisheria, kupata sifa ya kukopesheka na ukubalifu katika masoko ya ndani na nje;
(iv) Ushirikishwaji wa vikundi kwenye fursa ya kujitangaza, kuongeza wigo wa wateja, kubadilishana uzoefu na kupata masoko.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya ukuaji wa vikundi vya wanawake kiuchumi.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved