Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 7 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 67 2026-04-13

Name

Lucy Simirya Kombani

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. LUCY D. S. KOMBANI aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuboresha miundombinu kwa wakulima wanaolima milimani Mkoa wa Morogoro ili kudhibiti upotevu wa maji?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa wa miradi ya umwagiliaji katika Mkoa wa Morogoro ambapo katika mwaka wa fedha 2025/2026, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inatekeleza jumla ya miradi ya umwagiliaji 65.

Mheshimiwa Mwenyekiti, miradi inayotekelezwa ni pamoja na ujenzi wa Skimu ya Rudewa - Kilosa yenye ukubwa wa hekta 2,500 ambapo utekelezaji wake umefikia 41% na ujenzi unaendelea. Kukamilika kwa skimu hiyo, kutanufaisha wakulima 3,384 katika maeneo ya Kijiji cha Gongoni, Rudewa - Mbuyuni, Rudewa - Batini na Peapea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile, Serikali inaendelea na ukarabati wa Skimu saba za Mgongola, Tulokongwa, Itete, Mbalangwe, Kiroka, Msolwa - Ujamaa na Mvumi, ambapo utekelezaji umefikia wastani wa 45% na skimu za umwagiliaji 32 na mabwawa ya umwagiliaji 10 yapo katika hatua ya usanifu kwa zaidi ya 50%.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji itaendelea na jitihada za kuboresha miundombinu ya umwagiliaji hususan katika maeneo ya milimani ili kudhibiti upotevu wa maji na kuongeza ufanisi wa matumizi yake pamoja na uzalishaji katika kilimo.