Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2025-2030 | Session 3 | Sitting 7 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) | 61 | 2026-04-13 |
Name
Boniphace Mwita Getere
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bunda
Primary Question
MHE. BONIPHACE M. GETERE aliuliza: -
Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Shule ya Amali Manchimweru?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Boniphace Mwita Getere, Mbunge wa Jimbo la Bunda Vijijini, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuboresha elimu ya mafunzo ya amali kwa ngazi ya sekondari, Serikali katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali ilitoa shilingi bilioni 88.84, kwa ajili ya ujenzi wa shule 103 za amali za kihandisi ambapo shule 29 zilipokea fedha za ujenzi wa miundombinu yote.
Mheshimiwa Mwenyekiti, shule 74, ikiwemo shule ya Manchimweru, Wilayani Bunda, zilipokea fedha za ujenzi wa miundombinu kwa awamu ya kwanza. Shule hii ilipokea shilingi milioni 584.28 ambapo ujenzi wake umefikia 92% na tathmini inaonesha kiasi cha shilingi milioni 950 kinahitajika ili kukamilisha ujenzi kwa awamu ya pili.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa shule hizi unafanyika kwa awamu, na hivyo, shule ya sekondari ya Manchimweru itapelekewa fedha za ukamilishaji mara utekelezaji wa awamu ya pili utakapoanza, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved