Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2025-2030 Session 3 Sitting 3 Natural Resources and Tourism Wizara ya Maliasili na Utalii 18 2026-04-02

Name

Asma Ali Mwinyi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Welezo

Primary Question

MHE. ASMA ALI MWINYI aliuliza:-

Je, Serikali ya Muungano na Zanzibar zina mpango gani wa kuunganisha na kukuza Utalii nchini kuzingatia bajeti, miundombinu na fursa za ajira?

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Asma Ali Mwinyi, Mbunge wa Welezo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kuunganisha na kukuza utalii nchini kupitia mifumo ya Serikali, Wizara ya Maliasili na Utalii, Tanzania Bara na Wizara ya Utalii na Mambo Kale Zanzibar, zimekuwa na utaratibu wa Mikutano ya Ushirikiano. Mikutano hiyo imekuwa jukwaa muhimu katika kujadili kwa pamoja mustakabali wa maendeleo ya utalii, kuongeza ufanisi wa utekelezaji wa masuala ya kisera na usimamizi wa sekta ili kuhakikisha utalii unaleta tija zaidi kwa Taifa letu.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile, kumekuwa na jitihada za pamoja katika eneo la utangazaji utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZCT) ambazo zimesaini Hati ya Makubaliano inayolenga kuimarisha ushirikiano wa utangazaji utalii wa Tanzania kama kituo kimoja.

Mheshimiwa Naibu Spika, taasisi hizo zinaendelea kushirikiana na Sekta Binafsi kutangaza vivutio na mazao ya utalii yaliyopo nchini kupitia matukio ya Kimataifa yakiwemo Swahili International Expo-S!TE, KaribuKili Fair, Z-Summit, ITB Berlin na WTM London. Halikadhalika, kushirikiana na nchi nyingine katika kukuza utalii endelevu kupitia majukwaa ya Shirika la Utalii Duniani (UN Tourism), Baraza la Usafiri na Utalii (WTTC), sambamba na Ushirikiano wa Kikanda kupitia EAC na SADC.